
Watu sita wamefariki katika ajali ya gari aina ya Prado lenya namba T 647 CVR, iliyotokea mpakani mwa wilaya za Mbinga na Nyasa kwenye eneo la Chunya leo Disemba 28, 2024.
Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili asubuhi imesababisha vifo vya walimu wanne wa shule ya msingi Lumaru, mfamasia mmoja na dereva wa gari hilo waliokuwa wakienda katika shule ya sekondari Limbo iliyopo wilayani Nyasa kwa ajili ya kufanya masaili ya watendaji, uboreshaji upigaji kura.
Kwa mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa aliyemwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Salumu Mohamedi amesema ajali hiyo imetokana na gari kuanguka katika mteremko wa chunya wilayani Mbinga na kuwaka moto.