×

Putin aomba radhi baada ya ajali ya ndege ya Azerbaijan iliyoua watu 38

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba radhi kwa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev kufuatia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan nchini Kazakhstan iliyosababisha vifo vya watu 38 katika anga ya Russia na ametoa pia salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na amewatakia waliojeruhiwa kupona haraka,” Kremlin ilisema katika taarifa.

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.

Hayo yakiarifiwa, mashirika kadhaa ya ndege yametangaza kusitisha safari za ndege kuelekea miji ya Russia, baada ya wataalamu kutoka nchi za Magharibi na Marekani kudai kuwa ndege ya Azerbaijan inaweza kuwa imetunguliwa na kombora la Russia.

Moscow imejizuia kutoa maelezo kuhusu ripoti kwamba ndege hiyo ilitunguliwa kwa bahati mbaya na mifumo ya ulinzi wa anga ya Russia.

Russia ilisema, mji mkuu wa Chechenya wa Grozny, ambako ndege hiyo ilitarajiwa kutua, ulikuwa umeshambuliwa siku hiyo na ndege zisizo na rubani za Ukraine.

Ndege hiyo ilianguka siku ya Jumatano karibu na mji wa Kazakhstan wa Aktau, na kuua watu 38 kati ya abiria 67

ZUCHU AVAMIWA JUKWAANI AONYESHA KITU CHA AJABU SANA – WALINZI WASTAAJABU….

Leave a Comment