×

Madonna Avishwa Pete na Kiserengeti Boy Chake Akiwa na Umri wa Miaka 66

Si huwa wanasema age is nothing but numbers wakimaanisha umri si chochote bali ni namba tu? Basi mkongwe wa muziki wa Pop duniani, mwanamama Madonna amedhihirisha kwa vitendo.

Akiwa na umri wa miaka 65, Madonna amevishwa pete ya uchumba na Kiserengeti boy chake, Akeem Morris chenye umri wa miaka 28! Piga hesabu hapo ya tofauti ya huo umri, bado huamini kama age is just numbers?

Katika picha anazoshea kwenye mitandao ya kijamii, Madonna anawaringishia wavimba macho pete yake hiyo ya diamond aliyovalishwa ambapo unaambiwa kila picha anayopiga, lazima mkono wenye pete uoneshwe kwa makusudi kabisa.

Madonna amewahi kuolewa mara mbili, mara ya kwanza na mwigizaji Sean Penn kuanzia mwaka 1985 hadi 1989 na baadaye na dairekta Guy Ritchie kutoka 2000 hadi 2008 ambapo amewahi kunukuliwa akisema anazijutia ndoa zake zote mbili.

Leave a Comment