
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amekabidhi gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya Kome ambapo litasaidia kutoa huduma kwa wakazi wa Kata za Buhama, Bugoro, Lugata na Nyakasasa.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Kome, Shigongo amewaomba wananchi hao kuunga mkono serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili.