×

Askari Magereza Jela Kwa Kufanya Mapenzi na Mfungwa

Askari magereza katika Gereza la HMP Wandsworth jijini London, Uingereza, Linda De Sousa Abreu

Askari magereza katika Gereza la HMP Wandsworth jijini London, Uingereza, Linda De Sousa Abreu, 31, amehukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mfungwa wa kiume ndani ya selo katika gereza hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa, Juni 25, 2024 akiwa zamu katika Gereza la HMP Wandsworth, aliingia kwenye selo ya mfungwa wa kiume na kufanya kitendo hicho ambacho kilirekodiwa na mfungwa mwingine kabla ya video ya tukio hilo kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Juni 28, 2024, mwanadada huyo mrembo alikamatwa na polisi katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow akijaribu kutoroka kuelekea Madrid, Hispania baada ya video zake kusambaa mitandaoni.

Katika hukumu iliyosomwa jana, Januari 6, 2025 katika Mahakama ya Isleworth Crown Court, Jaji Martin Edmunds aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alinukuliwa akisema kuwa Afisa magereza huyo alikuwa anatambua kwamba kitendo alichokuwa anakifanya ni kinyume cha sheria lakini akaamua kufanya.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, askari magereza huyo kabla ya kurekodiwa na video kusambaa mitandaoni, alikuwa ameshafanya mapenzi na mfungwa huyo kwa takribani mara tatu au nne katika siku tofauti kabla ya siku ya tukio.

Leave a Comment