×

AY: Kumbe kolabo na Lil Romeo lilimtoa kimataifa!

aytanzaniaAmbwene Yesaya ‘AY’.

WIKI iliyopita tuliishia pale msanii AY aliposema kuwa mwaka 2010 ulikuwa wa neema kwake kwani alifanikiwa kuchaguliwa katika kuwania tuzo mbalimbali pamoja na kujishindia baadhi yake zikiwemo Tuzo za Kimataifa za Redio Ufaransa (International Radio France) na kuahidi kuendelea kukuelezea zaidi tuzo zake nyingine ambazo aliwahi kuzipata.

Songa naye…

Kama nilivyoeleza kuwa mwaka 2010 ulikuwa wa neema kwangu hata hivyo tuzo ziliendelea kumiminika, mwaka 2011 nilipochaguliwa kushiriki katika Tuzo ya Pearl Africa Music nchini Kenya katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume kutoka Tanzania ambapo nilishinda tuzo hiyo. Nikashinda tuzo nyingine ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki iliyotolewa na East African Music 2011.

“Mwaka 2012 nikashinda Tuzo ya Video Bora Afrika Mashariki kupitia Channel O Video Music Awards na kunifanya kuwa na idadi ya tuzo zaidi ya 17 huku nyimbo ‘zilizo-hit’ kufanya vizuri kwa kushika chati mbalimbali zikiwa ni 32, baadhi ya nyimbo hizo ni Party Zone niliomshirikisha prodyuza kutoka MJ Records, Marco Chali ambaye pia alihusika katika kuute-ngeneza. Pia akanite-ngenezea  Wimbo wa Money niliomshi-rikisha Vanessa Mdee ‘Vee Money.

“Nyimbo hizo zilinitambulisha vizuri sehemu kadhaa za dunia na baadaye nikafanikiwa kufanya Wimbo wa Speak With Ya Body kwa kumshirikisha Star wa muziki kutoka Hollywood nchini Marekani, Lil Romeo na Lamyia. Wimbo huo ulipata nafasi ya kuchezwa sana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni kubwa kubwa ikiwemo Trace ya nchini Ufaransa, MTV ya nchini Marekani na Channel O ya Afrika Kusini naweza kusema kuwa ni moja ya kolabo ninalojivunia kunitangaza kimataifa.

“Pia nimefanikiwa kushirikiana na wasanii wengi wa Afrika Mashariki na nje ya Afrika ambao baadhi yao ni Jose Chameleone, Ngoni (Uganda),

Amani, Name-less, Juacali (Kenya), P. Square (Nigeria), Miss Trinity na Sean Kingston (Jamaica) ambaye nilishi-rikiana naye kwenye Wimbo wa Touch Me, Fuse ODG &Young

Joc kutoka kwenye lebo ya msanii maarufu wa Kimarekani, Sean John Combs ‘ P. Diddy (Bad Boy Entertainment, Puffy Daddy’s Label).

Jina langu likazidi kukua na kufanikiwa kuwa balozi wa makampuni  mbalimbali nchini  ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Airtel Tanzania, Coca Cola, Samsung, Malta Guiness, Mfuko wa Shirika la Umoja wa Mataifa  ‘Unicef’ linalohusika na watoto.

“Mpenzi msomaji wa makala haya, nimeelezea mambo mengi sana kuhusu maisha yangu halisi ikiwemo changamoto, kuthubutu, kujituma, mafanikio na kadhalika.

 Wiki ijayo nitazungumzia maisha yangu ya uhusiano, naomba uungane nami.

Kama una maswali au maoni yatume kupitia namba ya mwandishi nami nitayajibu.

Leave a Comment