×

OFM Kazini Yamnasa Mke wa Mtu Akichepuka

chepuka-(1) chepuka-(2)DAR ES SALAAM! Kumbe kuchepuka hakuna umri bwana! Mwanamke ambaye jina linapigwa ‘tinted’ kwa sasa, Ijumaa     iliyopita alinaswa akiingia kwenye gari la mwanaume anayedaiwa ni mchepuko wake na kwenda kusikojulikana baada ya kufuatiliwa kwa karibu na shemeji yake akishirikiana na makamanda wa kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, lisikilize Amani.

ENEO LA TUKIO

Tukio hilo la ‘aibu yake’ lilijiri saa 6:00 mchana wa siku hiyo kwenye maegesho ya maduka makubwa ya Mlimani City jijini Dar.

SIMU OFM

Ilikuwa saa 5:17 asubuhi, simu iliingia kwenye chumba cha habari ambapo mpigaji alisema yeye anaitwa Dadi. Alisema ana shemeji yake (mke wa kaka yake) amekuwa akichepuka sana, hasa kipindi hiki ambacho kaka yake amekwenda kikazi nchini Marekani.

SIKIA SIMULIZI

“Huyu shem, karibu kila siku anachepuka. Na akitaka kwenda kwenye michepuko yake inaanza kuingia simu, akiongea utasikia ‘i miss you’, ‘me too honey’. Baadaye anauliza ‘wapi’, ‘basi nakuja sasa hivi’. Halafu anajiandaa na kuondoka. Mi inaniuma sana kwani bro (kaka) ameacha pesa ya kutosha na ikibidi huwa tunakwenda kuchukua kwenye biashara zake, Sinza (Dar).

“Sasa leo muda huu, kapokea simu. Nikamsikia akisema najiandaa sasa hivi. Nitapanda Bajaj hadi pale nje Mlimani City, nitaingia na geti la barabara kubwa. Nitakupigia.

“Jamani kama kweli ninyi ni OFM, naomba tukutane pale muda huu, ndiyo ametoka kama dakika tano tu. Mi naumia sana. Nimemuuliza safari ya wapi shem, akasema anakwenda kwenye Vicoba, lakini mi najua hana cha Vicoba wala vifurushi,” alisema shemeji mtu huyo.

OFM YAJIPANGA

Baada ya maelezo hayo, OFM walijiteua, baadhi ya makamanda walikwenda Mlimani City na kukutana na Dadi ambaye alisema:

“Naamini hajafika, ila sasa kwa sababu atashuka nje ya geti, sisi tukaeni humuhumu ndani, akiingia nitawaonesha. Mi naumia sana kwa kweli. Bro akijua hakuna ndoa tena.”

BAADA YA DAKIKA 20

Zilipokatika dakika 20 huku OFM na Dadi wakirandaranda ndani kwenye maegesho, jamaa huyo alimwona shemeji yake akiingia kwenye geti linalotazamana na Barabara ya Sam Nujoma.

“Eheee! Yule anakuja, amevaa t-shirt na suruali ya kitambaa chenye mauamaua,” alisema shemeji mtu.

OFM YATEGA KAMERA

Kwa vile Dadi alisema haoni sababu ya kumfumania shemeji yake kwa kuwa yeye si mume. Aliomba apigiwe picha za kumwaga ili iwe ushahidi siku likitokea la kutokea.

Ilibidi OFM wajipange mara tatu. Mmoja alikaa ndani na kamera ya kuvuta kwa mbali, wa pili alikwenda kusimama geti aliloingilia mwanamke huyo na wa tatu alitoka nje na kwenda kusimama kwenye geti la kutokea kwenye Baa ya DDC.

Mwanamke huyo, aliingia kwenye gari aina ya Toyota Prado ambapo dereva wake alikuwemo ndani kwa muda kisha wakaondoka kupitia geti la kwenye Baa ya DDC. Lilikata kulia na kushika mzunguko wa magari kwa kuelekea Mwenge.

MASWALI NA DADI

OFM: “Wewe una uhakika gani kama yule ni mchepuko wa shemeji yako?”

Dadi: “Shemeji hafanyi kazi, hafanyi biashara. Yule ni nani sasa? Japokuwa sijamwangalia sawasawa kwa sababu nilijificha lakini simjui. Na kama kweli alikuwa anakuja kwenye Vicoba kwa nini wametoka hata bila kukaa kule kwenye meza?

OFM: “Kawaida akitoka muda huu huwa anarudi saa ngapi nyumbani?”

Dadi: “Nne, tano usiku, tena akiwa amelewa chakari.”

OFM: “Mnaishi wapi?”

Dadi: “Sinza, Mugabe. Yaani mtaani ni aibu tupu. Kila mtu anajua shemeji yangu mchepukaji. Namwomba Mungu bro arudi salama akutane nayo mwenyewe.”

MADAI YALIVYO

Kumekuwa na madai kwamba, eneo hilo la maegesho ya Mlimani City hutumiwa na watu wenye kuvunja uaminifu wa kimapenzi. Wengi huingia humo na kuwasubiri  wanaochepuka nao kisha kuondoka badala ya kuwasubiri mitaani.

Imeandikwa: Chande Abdallah na Boniphace Ngumije.

Leave a Comment