Nyota wa Bongo Flava na Amapiano, Harmonize, ameachia wimbo wake mpya Furaha, ambao umetikisa mitandao ya kijamii si kwa ladha yake tu, bali pia kwa video yake yenye mvuto wa kipekee.
Katika video hiyo, Harmonize anaonekana akiwa na msanii chipukizi anayechipukia kwa kasi, Abigail Chams. Wakiwa kwenye mandhari maridadi, wawili hao wanaonyesha uhusiano wa karibu wa kimuziki, wakiburudisha mashabiki kwa dansi la kusisimua na mahadhi yanayoshika hisia.
Kwa mashabiki wa muziki wa mapenzi, Furaha ni wimbo unaofaa kabisa kuwa sauti rasmi ya Valentine’s Day mwaka huu!