
Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas Tanzania usiku wa kuamkia leo imeibuka kinara wa jumla katika Tuzo za Tehama zilizoandaliwa na mamlaka ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano TEHAMA.
Katika Tuzo hizo Yas imeibuka mshindi wa jumla kwa makampuni yanayoongoza kwa matumizi ya Teknolojia ya habari Tehama, ambapo imekuwa ikishindanishwa na makampuni mengine yanayotoa huduma kwa jamii.
Yas imekuwa kinara kwenye matumizi teknolojia ambapo imekuwa ikijikita zaidi katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo data, mawasiliano ya simu, pamoja na jumbe fupi sms.
Mwishoni mwa mwaka jana kampuni ya Yas iliweza kuibuka kinara na hatimaye kutwaa tuzo ya mshindi wa jumla Africa, tuzo hizi zinazoandaliwa na shirika la kimataifa la OOKLA lenye maskani yake nchini Marekani ambapo Yas, ilifanikiwa kuibuka mshindi mara mbili wa tuzo hiyo.