×

Martha Mwaipaja Avunja Ukimya Kuhusu Mashambulizi Dhidi ya Binti Yake

Staa wa muziki wa Gospel, Martha Mwaipaja

Staa wa muziki wa Gospel, Martha Mwaipaja, amekuwa akizungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na masuala ya kifamilia kati yake, mdogo wake Beatrice Mwaipaja, na mama yake mzazi. Katika post aliyoiandika kwenye Instagram hivi karibuni, Martha ameonyesha hasira na machungu kuhusu mashambulizi anayoyapata mtoto wake, Joanitha (Joani), akishangazwa na namna watu wanavyoshambulia maisha yake binafsi.

Joanitha (Joani)

Martha amesema:
“Leo ningependa kusema jambo kuhusu mtoto wangu Joanitha. Mnaomtukana binti yangu, na nani kasema kwamba Joan si mtoto wangu? Mimi ndio mama yake, na hata dunia itageuka, nitabaki kuwa mama yake milele. Acheni kumtukana mtoto wangu; kila mtu ana familia yake na maisha yake. Kila mtu aishi maisha yake. Kesho ya binti yangu ipo mikononi mwa Mungu na mikononi mwangu. Hakuna anayemfahamu mtoto wangu zaidi yangu. Nimenyamaza kwa muda sasa, lakini acheni kumgusa mtoto wangu. Nakupenda sana binti yangu.”

Hii ni wazi ni ujumbe wa kutetea familia yake, hususan mtoto wake, na kusema kwamba hawezi kuvumilia kuona mtoto wake akishambuliwa. Anataka watu waheshimu familia yake na kumwacha aishi kwa amani.”