
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Wilbert Mica Siwa Februari 26, 2025 amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kufanya doria ya magari na miguu kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji Mbeya.

Kamanda Siwa ameeleza kuwa lengo la doria hiyo ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao ikiwemo usalama barabarani kwa watumiaji wa barabara hasa katika maeneo yote tete ya Milima Iwambi, Igawilo na Mlima Nyoka ili kudhibiti ukiukwaji wa sheria za barabarani.
Aidha, Kamanda Siwa ametanabaisha kuwa Jeshi hilo limejipanga vizuri kuzuia uhalifu wa aina yoyote ile na amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuzuia na kutokomeza uhalifu.


