Mkutano wa G20 uliokuwa ukifanyika nchini Afrika Kusini umemalizika jana bila ya washiriki wake kufikia mwafaka.
Afrika Kusini ambayo ni nchi ya 21 imesikitishwa na hatua ya kumalizika kwa mkutano wa G20 kuhusu uchumi wa dunia bila kupatikana mwafaka baada ya maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi kadhaa kukwepa na wajumbe wengine kujiweka mbali na masuala ya kufadhili mabadiliko ya tabianchi.
Mkutano wa siku mbili wa G20 uliokutanisha mawaziri wa fedha na benki kuu mjini Cape Town Afrika Kusini ulishindwa pia kutoa taarifa ya pamoja.
Hata hivyo taarifa fupi ya mwenyekiti iliyotolewa na mwenyeji wa mkutano huo ilisema washiriki walisisitiza kupinga sera ya kiuchumi inayozuia uagizaji bidhaa kutoka nje ya kundi hilo.
Muhtasari huo uliongeza kuwa, waliunga mkono mfumo wa biashara wa kimataifa unaozingatia kanuni, usio na ubaguzi, wa haki, shirikishi, endelevu na wa wazi, wakitumia maneno ambayo utawala wa Rais Trump tayari umepinga vikali.
Lakini mazungumzo yaligubikwa na kukosekana kwa wadau muhimu wa fedha – kama vile Marekani, China, India na Japan – na kupunguzwa kwa misaada kwa taifa lenye uchumi mkubwa kama Marekani na Uingereza.