
Zaidi ya watu 20 wamefika katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam Machi 4, 2025 wakidai kutapeliwa na muigizaji maarufu nchini, Nicole Joeberry, kupitia mchezo wa upatu mtandaoni.
Waathiriwa hao wanadai kuwa Nicole alitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuanzisha mchezo wa upatu, na kutokana na umaarufu wake, waliamini na kushiriki katika mpango huo.

Hata hivyo, baada ya kushiriki bila mafanikio, walipojaribu kufuatilia mrejesho wa fedha zao, hawakupata majibu yoyote, na baadaye waligundua kuwa Nicole alikuwa amewazuia kwenye mitandao yake.
Taarifa zinaeleza kuwa Nicole tayari yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.