×

Kamati ya Bunge yamshukuru Rais Samia kwa kuinua Sekta ya Michezo nchini

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Husna Sekiboko imekagua mradi wa ujenzi wa eneo Changamani la Michezo Dar es salaam (Benjamini Mkapa na Uhuru)Machi 15, 2025 jijini Dar es Salaam ambapo imemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utashi wake katika kusaidia kuinua sekta ya Michezo nchini.