
Hapo jana, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, alimuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa mizani waliokuwa zamu katika mizani zilizopo kwenye barabara kuu ya T1 inayoanzia Dar es Salaam – Zambia kupitia mpaka wa Tunduma, kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa malalamiko katika mizani hizo.
Ulega alifanya maamuzi hayo mara baada ya tukio lililotokea hivi karibuni, ambapo msafirishaji Bi. Pamela James Bukumbi, mwenye gari la mizigo namba T 137 DLQ likiwa na tela T 567 CUR, alilalamikia kutozwa faini ya kuzidisha uzito katika mizani ya Vigwaza, wakati mizani nyingine alizopita gari yake haikuwa imezidisha uzito.
Huyu ndiye Pamela Bukumbi, mwanamke aliyeibua malalamiko hayo!