Rais Dkt. Samia Apokea Taarifa Ya Mwaka Ya Takukuru Na CAG 2023/2024 – (Picha + Video)
Global Publishers March 27, 2025
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Crispin Chalamila kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi, 2025.
Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Akipokea Taarifa ya Mwaka ya TAKUKURU na Ripoti ya CAG kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Ikulu Dar es Salam, leo tarehe 27 Machi, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023/24 kutoka Charles Kichere kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi, 2025.
Rais Samia akiwa na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kupokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023-2024 pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ikulu Jijini Dar es Salaam