
KATIUBU wa CCM Mkoa Mwanza Omari Mtuwa amewaonya makada wa chama hicho wanaojipitisha kusaka ubunge na Udiwani kabla muda kuwa chama kitawashughurikia.
Kauli hiyo ameitoa wilaya ya Magu alipokutana na wajumbe wa Sekretalieti ya Kata ya Matawi Wilayani humo.
Mtuwa amesema kumekuwa na tabia ya makada wa CCM Mkoa Mwanza ambao wameanza kampeni za kusaka ubunge na Udiwani kwenye majimbo yaliyoko Mkoa wa Mwanza kabla ya wakati huku wakijua kufanya hivyo ni kosa chama Kiko macho hakitasita kuchukuwa hatua za kinidhamu juu yao.

Amesema muda wa kampeni bado hivyo chama bado kinawatambua wabunge na madiwani walioko madarani Kwa sasa wanatakiwa kuachwa na kutekeleza majukumu yao ya kutekeleza ila ya CCM.
Huku akitoa maelekezo kwa watendaji wa Chama hicho kuacha tabia ya kukumbatia Wagombea na kuwatembeza Kila mahali ili kusaka kukubalika kwa wanachama jambo hilo halikubaliki.
