
Sakata la mwanamke Neema Kilugala, kudai kubadilishiwa mtoto na kupewa aliyefariki dunia baada ya kujifungua, limechukua sura mpya baada ya majibu ya DNA kutoka ambapo inaelezwa kuwa vinasaba vya mwanamke huyo na mtoto anayemkataa ambaye alifariki dunia, vinafanana kwa asilimia 99.9.
Mwanamke huyo alidai kuwa alijifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, mnamo Machi 24, 2025 kisha akabadilishiwa mtoto na kupewa aliyefariki dunia.
Majibu hayo yanaonesha kwamba hakukuwa na kubadilishwa kwa mtoto na anayemkataa kuwa siyo mwanaye, ndiye mwanaye aliyemzaa.