
MSHAMBULIAJI Jonathan Sowa mali ya Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani balaa lake limezidi kuwa zito kutokana na kasi yake uwanjani.
Mshambuliaji huyo rai awa Ghana anatajwa kuwa kwenye rada za mabingwa watetezi wa ligi namba nne kwa ubora Afrika, Yanga ni chaguo la kwanza ndani ya timu ya Singida Black Stars.
Kwenye mechi 8 ambazo amecheza kwenye ligi ni mabao 8 kafunga akiwa katika mwendelezo bora na miongoni mwa makipa ambao aliwatungua Djigui Diarra anaingia kwenye orodha.

Katika mchezo uliochezwa Aprili 2 2025 Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa, Manyara wakati ubao ukisoma Fountain Gate 0-3 Singida Black Stars dakika ya 29 alipachika bao la uongozi, Frank Kwabena dakika ya 56 alipachika bao la pili na kamba ya tatu ikapachikwa na Emmanuel Kwame dakika ya 71.
Singida Black Stars inafikisha jumla ya pointi 47 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya mechi 24 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 35 msimu wa 2024/25.
Fountain Gate inakuwa timu namba moja kufungwa mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 43 baada ya mechi 24 ikiwa nafasi ya 7 kwenye msimamo na pointi 28.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga wanafuatilia kwa ukaribu mwendo wa Sowa ambapo mipango ikienda sawa atakuwa ni njano na kijani msimu wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.