×

Waziri Mkuu na Naibu Wake Washiriki Kikao cha Kwanza Bunge la Bajeti leo – Picha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 8, 2025 ameshiriki Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge Bunge jijini Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Aprili 8, 2025, ameshiriki kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge, kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.

Ushiriki wa Waziri Mkuu unadhihirisha mwendelezo wa usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za serikali bungeni, huku kikao hicho kikitarajiwa kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Wabunge mbalimbali mara baada ya kuahirishwa mkutano wa kumi na tisa wa Bunge, Kikao cha kwanza April 8, 2025 Jijini Dodoma.