
Klabu ya Simba SC imepokea zawadi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa kampeni ya Goli la Mama, mara baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kimataifa. Ushindi huo ulipatikana kupitia mikwaju ya penati dhidi ya timu ya Al Masry ya Misri.
Kampeni ya “Goli la Mama” imekuwa ikitoa motisha kwa wachezaji huku pia ikionesha namna ambavyo mashabiki na wadau wa michezo wanavyojivunia mafanikio ya timu zinazoshiriki katika ngazi ya kimataifa.
