Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, wamepokea Press Jackets toka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Kwa ajili ya usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwenye kujua sheria za kuripoti habari kipindi cha uchaguzi, ambayo yamefanyika Mei, 2, 2025 jijini Dar-es-Salaam, Mratibu wa THRDC Onesmo Olengurumwa amesema kuwa ni wajibu wa Mwandishi kuandika na kuripoti taarifa zilizo sahihi ili kuepuka kuingiza nchi katika machafuko.
“Ni muhimu kufanya kazi katika mazingira salama na pia kuandika habari kwa Uhuru na Usalama tunavyoelekea katika uchaguzi mkuu ambao unaotarajiwa kufanyika mwaka huu,2025
na tunatoa majaketi haya ili iwe rahisi kutambulika kama ni muandishi na kufanya kazi Yako kwa weredi,” amesema.