×

Vyama vya siasa vyapigwa marufuku kufanya siasa Mali

Mamani Nassire

Serikali ya kijeshi nchini Mali imetangaza kusitisha shughuli za vyama vyote vya kisiasa na mashirika ya kiraia katika taifa hilo la Afrika Magharibi linalokumbwa na mzozo wa kisiasa.

Waziri anayehusika na mageuzi ya serikali, Mamani Nassire, ametangaza uamuzi huo kupitia taarifa iliyotolewa kwenye televisheni ya taifa wakati wa mkutano usio wa kawaida wa Baraza la Mawaziri.

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwepo na jaribio la mara kwa mara la kupinga kusitishwa kwa shughuli za vyama vya kisiasa nchini humo. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeukosoa uamuzi huo, likisema ni pigo jingine kwa demokrasia nchini Mali.

Mnamo April mwaka huui, mawaziri walipendekeza muda wa kiongozi wa kijeshi Assimi Goita uongezwe muda hadi mwaka 2030. Goita ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka 2020 na 2021, ameahidi kuandaa uchaguzi japo mipango hiyo imeahirishwa kwa “sababu za kiufundi” bila ya kutolewa muda maalum wa kufanyika kwa uchaguzi huo.

Kulingana na tangazo hilo la Mamani, watu wanaohudumu katika taasisi za kisiasa na kiutawala za Serikali kwa sababu ya kuteuliwa kisiasa wanaweza kuendelea na majukumu yao, lakini bila kudai kuwa ni sehemu ya chama chao.

Serikali ya mpito inabainisha kuwa hatua hii inafuatia kufutwa kwa mkataba wa vyama vya siasa. “Tuko katika mchakato wa mageuzi,” ameeleza Mamani Nassiré, akibainisha kuwa mchakato huo utaendelea. Itabidi sheria mpya itungwe hasa kwa ajili ya usimamizi wa maisha ya kisiasa ya Mali.

Miongoni mwa malengo yaliyowasilishwa tayari ni pamoja na kupunguza idadi ya vyama vya siasa vilivyoidhinishwa, kuimarisha sheria za kuunda vyama vipya, kuzuia au hata kupiga marufuku ufadhili wao wa umma.

Katika wiki za hivi karibuni, vyama vya siasa vya Mali viliendelea kushutumu kufutwa kwao kuliopangwa, ambao wanachukulia kuwa ni ukiukaji wa Katiba na shambulio dhidi ya wingi na mafanikio ya kidemokrasia. Vuguvugu la maandamano ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini humo lilizuka mapema mwezi huu, lakini baadhi ya viongozi wake kadhaa wametekwa nyara na Usalama wa Taifa katika siku za hivi karibuni, na kuwanyamazisha wanaharakati wanaounga mkono demokrasia.

Stori na Elvan Stambuli, GPL

MSAJILI AILIPUA CHADEMA-MCHOME ACHEKELEA-NI BAADA ya KUSHINDA KESI-GOLUGWA AKAMATWA AIRPORT