×

Betika Mwendo Uleule Kuwafikia Wasomaji Wake

 

MAPEMA leo Jumatano, Aprili 29 mwaka huu timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Buguruni, Malapa na maeneo ya Rozana ambapo wasomaji wa gazeti la betika wamejichukulia  nakala ya gazeti hilo.

 

Wasomaji  hao wameonesha furaha yao kukutana na timu ya maofisa masoko, ambapo walijipatia gezeti hilo ambalo ni mahususi katika masuala ya kubeti na habari mbalimbali zinazotokea katika pande za nchi hii.

Mbali na masuala ya kubeti pia hutangaza biasha mbalimbali za watu ambao tayari wanavutiwa na uwepo wa gazeti hilo.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Leave a Comment