
Staa wa Hip Hop, Venance Mabeste.
ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu mastaa wa Muziki wa R&B Bongo, Bernad Paul ‘Ben Pol’ pamoja na Juma Musa ‘Jux’ kuachia ngoma ya Nakuchana, staa wa Hip Hop, Venance Mabeste naye anatarajiwa kuja na Ngoma ya Nakuchana Leo.
Akizungumza na Showbiz Xtra, Mabeste aliyewahi kubamba na Ngoma ya Baadaye Sana alisema kuwa ngoma hiyo aliipika muda mrefu ndani ya Studio za Switch Records chini ya Prodyuza Rufa na kwamba ilikuwa ikisubiriwa siku ya kuiachia tu.
“Ngoma yangu na ile ya kina Jux na Ben Pol kwanza niliipatia jina mapema kabla ya Nakuchana ya kina Jux pili mashabiki waelewe kwamba ni vitu viwili tofauti, wale wameimba na mimi nimechana, hata ukiisikia bado havifanani, next week ngoma itakuwa hewani,” alisema Mabeste.