
Singida Black Stars wamefuzu Fainali ya Kombe la CRDB FEDERATION CUP baada ya kuifunga Simba SC Bao 3-1 kwenye mchezo wa Nusu Fainali uliomalizika katika Dimba la Tanzanite Kwaraa Babati mkoani Manyara.
Sasa ni Rasmi Fainali ya Kombe hili itawakutanisha Yanga SC v Singida BS mwishoni mwa mwezi June, hii inamaana kwamba Yanga na Simba hawawezi kukutana tena msimu huu ikiwa Yanga watang’ang’ania kauli yao ya Hatuchezi ng’o baada ya kudai kwamba wapewe haki yao ya Mei 8 mwaka huu ambapo Simba walikacha mechi hiyo Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Singida Black Stars imetinga fainali ya kombe la FA ambapo watamenyana na Yanga Sc.
FT: Simba Sc 1-3 Singida Black Stars
⚽ 68’ Ahoua
⚽ 17’ Sowah
⚽ 35’ Keyekeh
⚽ 48’ Keyekeh
Stori: Elvan Stambuli, GPL