×

NHC Yaeleza Rais Samia Alivyofanikisha Kukamilisha Mradi wa Majengo ya Kisasa

Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Hamad Abdallah akizungumza na wanahabari na wahariri leo.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limeelezea jinsi lilivyokwamuliwa na Utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuliwezesha kukamilisha baadhi ya miradi yake ya majengo ya makazi na biashara na kufufua baadhi ya miradi ukiwemo mradi wa jengo la Golden Premier Residence.

Mradi wa Golden Premier Residence ulikwama kwa miaka nane lakini sasa umeanza kuendelezwa upya na ambapo wahariri hao katika ziara yao hiyo walimkuta mkandarasi wa jengo hilo akiwa kazini kuendelea na ujenzi.

Akizungumza na wanahabari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Hamad Abdallah amesema anaushukuru sana uongozi wa Rais Samia ambaye amekuwa akiupa ushirikiano mkubwa mradi huo na kuwawezesha kila ilipohitajika ili wananchi wapate makazi bora.

Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo walipata nafasi ya kuitembelea miradi ya nyumba za shirika hilo ambayo ni 711, Golden Premier Residence na Samia Housing Scheme pamoja na Morocco Square.

Mradi wa Golden Premier Residence
Wahariri walipofika kwenye mradi wa Seven Eleven (711)
Wahariri wakielekea kukagua mradi wa Golden Premier Residence.
Wahariri wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Hamad Abdallah alipokuwa akielezea miradi hiyo.
Mradi wa Samia Housing Scheme ambao umeshakamilika kwa asilimia 90.  HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL