
Mwanza, Tanzania – Juni 18 2025 — Benki ya Stanbic Tanzania imeshiriki katika Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Mwanza, ikionyesha dhamira yake ya kuendeleza ukuaji wa biashara za ndani kupitia suluhisho za kifedha zilizobuniwa mahsusi kwa ajili ya mahitaji ya wadau katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.

Benki hiyo iliwasilisha huduma bunifu ikiwemo Mikopo ya Magari na Vifaa (Vehicle and Asset Financing – VAF), Ufadhili wa Nishati Mbadala, pamoja na mitaji ya uendeshaji kupitia ufadhili wa mikataba, hususan kwa bidhaa za ndani zinazohusiana na makampuni makubwa ya sekta ya madini.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Bi. Mollen Charles, Meneja Mwandamizi wa Mahusiano anayehusika na Madini kutoka Stanbic Bank alisema:
“Tupo hapa kuiwezesha biashara ya Kitanzania kupitia suluhisho rahisi, zinazokua kulingana na sekta, na zenye kuleta matokeo chanya ya muda mrefu. Iwe ni kupata vifaa kupitia mikopo, kuhamasisha matumizi ya nishati safi au kusaidia mzunguko wa fedha kupitia mikataba, Stanbic ipo mstari wa mbele katika kusaidia ukuaji shirikishi.”
Ikiadhimisha miaka 30 ya uwepo wake nchini Tanzania, ushiriki wa Stanbic katika mkutano huu ni ushahidi wa nafasi yake endelevu katika kuchochea ajenda ya maendeleo ya taifa.
“Tanzania ni nyumbani kwetu, tunachochea maendeleo yake,” ni falsafa inayoongoza shughuli za benki katika kusaidia biashara kustawi na kupanuka.
Stanbic Bank inaendelea kujidhihirisha kama mshirika wa kweli kwa biashara katika sekta ya madini na sekta nyingine, sambamba na jitihada za kitaifa za kuongeza ushiriki wa Watanzania na kuwainua kiuchumi.