
Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Queen Fraison almaarufu kama Bonge la Dada, kwa sasa yuko kwenye moto wa kuotea mbali!
Kupitia mahojiano mafupi aliyofanya hivi karibuni, Queen Fraison amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi na ndiyo yeye mwenyewe alimtema mpenzi wake wa awali. Amedokeza kuwa hajutii maamuzi yake na kwa sasa anajipa muda wa kutulia na kujijenga zaidi.
“Nimeachana na mtu wangu, na ni mimi ndiye niliamua kumuacha. Nataka kupumzika kwanza, halafu baada ya miaka miwili nitaanza kufikiria tena kuingia kwenye mahusiano,” alisema kwa kujiamini.