
Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho.
Mchungaji Msigwa alijiunga na CCM mapema mwaka huu akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambako aliwahi kuwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa kipindi cha miaka 10.
Hatua yake ya kuchukua fomu inaibua ushindani mkali ndani ya chama hicho, hasa ikizingatiwa kuwa Jimbo la Iringa Mjini kwa sasa linashikiliwa na Mbunge Jesca Msambatavangu anayemaliza muda wake na ambaye ametangaza nia ya kutetea nafasi hiyo.
