×

Yamoto kutumbuiza kwenye uchangiaji damu Dar leo

yamoto band (8)Yamoto Band wakikamua wakifanya makamuzi kwenye jukwaa la Dar Live.

Stori:  Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais, Samia Salum Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Changia Damu Okoa Maisha linaloendelea leo katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Yamoto Band.

Changia-damu-new
Akizungumza na gazeti hili, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligeisha alisema Makamu wa Rais, Samia anatarajiwa kushiriki kutoa damu pamoja na viongozi wengine.

Alisema: “Lengo la tamasha hilo linaloitwa Changia Damu Okoa Maisha ni kukusanya lita kati ya 5,000 na 6,000 ambazo ni asilimia 75 ya mahitaji ya damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”

YAMOTO-BAND-2Alisema tamasha hilo kama linavyojieleza, kwamba wachangiaji wa damu watakuwa wanafanya hivyo ili damu hiyo ipelekwe benki ya damu kwa ajili ya wagonjwa watakaoihitaji.

Katika tamasha hilo, kutakuwepo na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza bure wakiwemo vijana wa Yamoto Band na THT ambao watafanya vitu vyao wakati zoezi hilo likiendelea.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, Clouds FM, Pepsi Tanzania, Startimes, Abbott Fund, Mfuko wa Pensheni wa GPEF, Benki ya CRDB, pamoja na Motsun Group Tanzania Ltd.

Leave a Comment