
Kampuni ya Stering katika Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya 49 mwaka huu yanayoendelea Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu Sabasaba imekuja na bidhaa mpya Blix ambayo ni teknolojia mpya ya uoshaji wa vyombo bila kutumia nguvu hivyo kuwa mkombozi wa usafi wa vyombo majumbani.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Stering, Lambert Kishoto amesema lengo lao kubwa la kufika kwenye maonesho hayo mwaka huu ni kuonesha bidhaa yao hiyo mpya ya Blix.

Ameendelea kusema kuwa bidhaa hiyo wameipeleka Sabasaba kwa ajili ya kuwaonesha wananchi teknolojia mpya ya uoshaji vyombo majumbani ikiwemo alminium za aina zote.
Lambert aliendelea kusema; “Naishukuru TanTrade kwa maandalizi mazuri na kuyafanya maonesho ya mwaka huu kuwa witikio mkubwa kuliko tulivyotegemea maana watu ni wengi mno wanaofika kwenye banda letu.
“Dhumuni lingine kubwa la Stering kuja kwenye maonesho haya ni kukutafuta wewe mdau wa usafi kuwa wakala wa bidhaa hizi ili usipate faida tu ya kutumia bidhaa zetu bali pia uweze kuwa wakala wetu ambaoi mpaka sasa wengi wameshajitokeza kwa ajili ya kuwa mawakala wetu.
“Ofisi zetu zipatikana sehemu mbalimbali hapa nchini lakini tumejigawa katika kanda nne na makao makuu yetu yanapatikana Arusha lakini tuna matawi Mwanza, Vingunguti Dar es Salaam na Mbeya katika Viwanja vya Nanenane.
“Ndugu mdau tunapozungumzia maosheo ya nyumbani Blix sasa ndiyo mkombozi wako.
Bidhaa hii hutengenezwa kiumahiri kabisa kwa kutumia nailoni pamoja na sponchi na hudumu kwa muda mrefu huku ukifanya usafi wa vyombo vyako bila kutumia nguvu.