×

Rais Samia Asalimiana Na Mbowe Baada Ya Uzinduzi Wa Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema  Freeman Mbowe mara baada ya kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.

Dodoma, Julai 17, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, mara baada ya kuzindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma.

Tukio hilo la kusalimiana limeonyesha ishara ya mshikamano na uzalendo miongoni mwa viongozi wa kisiasa nchini, hasa katika masuala ya msingi yanayohusu mustakabali wa Taifa.

Uzinduzi wa Dira ya 2050 umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, taasisi za kiraia, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo, ikiwa ni hatua ya kihistoria ya kuanza safari mpya ya maendeleo jumuishi ya muda mrefu.