×

Kiungo Hatari Kutoka Tunisia Balla Conte Ajiunga na Yanga

Kiungo wa zamani wa CS Sfaxien ya Tunisia, Moussa Balla Conte (21), sasa ni Mwananchi halali baada ya kusaini rasmi mkataba na Young Africans SC (Yanga).

Conte, ambaye alitua nchini asubuhi ya leo kwa ajili ya kukamilisha dili lake, amekamilisha taratibu zote na kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/25.

Nyota huyo alikuwa akiwaniwa pia na Simba SC, lakini Yanga wamefanikiwa kunasa saini yake na kumfanya kuwa sehemu ya kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ushindani wa ndani na kimataifa.