
Baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hali ya ndoa yao, hatimaye Barack Obama na Michelle Obama wamezungumzia wazi kuhusu mahusiano yao ya ndoa – wakikiri kuwa wamepitia changamoto lakini bado wanadumu katika upendo wa dhati unaowashikilia kwa karibu miongo mitatu.
Katika mazungumzo ya moja kwa moja kwenye podikasti ya IMO, inayohusisha Michelle pamoja na kaka yake Craig Robinson, wanandoa hao maarufu walivunja ukimya kuhusu uvumi wa mgogoro wa ndoa ambao umekuwa ukizungumzwa sana mitandaoni.
Wakiwa kwenye podikasti hiyo, Craig alifungua mada kwa utani: “Mnajipenda kweli?” Michelle akacheka na kujibu kwa mshawasha: “Ah ndio, zile tetesi zote.” Barack naye akachangia kwa mzaha: “Alinirudisha! Ilikuwa karibu kwisha.”