×

Mixx by Yas Yaja na ‘Kila Hatua Mixx’ Kuboresha Huduma za Kifedha

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx By Yas, Angelica Pesha akizungumza kwenye uzinduzi huo leo.

Dar es Salaam, 14 Agosti 2025: Mixx by Yas katika kuboresha huduma zake za kifedha leo imezindua kampeni yake mpya ya ‘Kila Hatua Mixx’ kampeni iliyokuja na mapinduzi makubwa ya uboreshaji wa huduma za kifedha.

Kampeni hiyo ambayo ni ya kitaifa imeanzia na jijini Dar es Salaam ambapo inatarajiwa kwenda kuzinduliwa kwenye kanda zingine inazotoa huduma.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliohudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, Wakurugenzi wa Yas na Mixx by Yas na wadau wengine Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas Angelica Pesha alisema;

“Tangu safari yetu ya utoaji huduma za kibunifu na zinazozingatia mahitaji ya Watanzania ianze mwaka 2010 mpaka leo tunajivunia mchango mkubwa na alama tunayoendelea kuiweka kwenye sekta ya fedha ikiwemo kuchochea Uchumi wa kidigitali.

 Wadau wakifuatilia matukio kwenye uzinduzi huo.
  • Tunawezesha Watanzania zaidi ya milioni 20 kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ya takribani shilingi trilioni 6 kwa mwezi.
  • Kupitia fursa za uwakala wa huduma za kifedha tunatoa ajira zisizo za moja kwa moja kwa mawakala zaidi ya 200,000 nchi nzima.
  • Vile vile, mifumo yetu ya kifedha inawezesha wafanyabiasha zaidi ya 500,000 kupokea malipo ya bidhaa na huduma kidigitali.
  • Pia makampuni binafsi pamoja na taasisi za umma zaidi 3,000 kukusanya na kufanya malipo ya mkupuo kwa wabia/suppliers na wafanyakazi wao.
  • Tumewezesha wateja zaidi ya milioni 6 kupata huduma za mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1 hivyo kufanya malengo yao kutimia.
  • Kuchochea utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwetu, tumewezesha watanzania kuweka akiba zenye thamani ya zaidi ya bilioni 600.

“Haya yote yamewezeshwa na maono, mikakati na nia yetu ya dhati ya kuchochea ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania wote. Tunawashukuru wateja, washirika wetu na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha na mawasiliano ambao wamekuwa nasi katika safari hii iliyojaa mafanikio na mchango chanya kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Tunatambua kuwa safari hii bado ni ndefu kwani bado kuna watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha mpaka sasa.

“Mixx tumejipanga kuendelea kubuni mikakati ambayo itachochea upatikanaji na utumiaji wa huduma za kifedha ikiwemo huduma za Mikopo, kuweka akiba, bima, uwekezaji ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na Tanzania ambayo kila mtu anafikia malengo yake bila kuwa na kikwazo cha kifedha.

“Mwisho niwakaribishe kwenye mjadala wa leo utakaongozwa na wataalam wa wadau wa huduma za kifedha ambapo kwa pamoja wataweza kutupa mikakati na suluhisho tunazohitaji ili kuongeza ujumuishwaji wa kifedha kutoka asilimia 76 ya sasa.

“Tunaamini teknolojia ni nguzo muhimu ya kufikisha huduma za kifedha maeneo mengi hapa nchini ikiwemo kuyafikia makundi maalumu kama vijana na wanawake. “Tupo tayari kusikiliza na kuchangia kwenye mjadala wa leo ili kuifikia Tanzania ambayo wote tunanufaika na Uchumi wa kidigitali. Alimaliza kusema Angelica kwenye uzinduzi huo.