
Mtaalamu wa mafunzo na vijana kutoka Vodacom Tanzania Plc,Bw Samwel Komba akimkabidhi cheti Mwanafunzi Doris Nisetasi, mhitimu wa mafunzo ya programu ya ‘Code Like A Girl’ yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo inafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika ijumaa jijini Dar es Salaam
Dar-es-Salaam, Septemba, 12, 2025, Vodacom Tanzania ikishirikiana na D Lab imewapa vyeti wasichana walioshiriki Program ya Code Like A Girl. Ambapo mpaka sasa mabinti zaidi ya 3370 nchini wamehitimu kwenye program hiyo inayolenga kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM)
Akizungumza na wanahabari mtaalamu wa mafunzo na vijana kutoka Vodacom Tanzania Plc,Bw.Samwel Komba amesema lengo ni kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike Katika masomo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) ambapo wasichana wanajfunza mambo mbali mbali ikiwemo kutengeneza website na siku ya leo wamewakilisha kile ambacho wamejifunza na kukionyesha.

Nae mmoja wa wanafunzi aliyehitimu mafunzo hayo Kurthum Hassan ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu amesema kuwa amefurahi kwa Kampuni ya Vodacom Tanzania kuwapatia mafunzo hayo kwa sababu wamepata kujifunza namna ya kutumia Komputa kwa undani zaidi kupitia mafunzo ameweza kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo kutengeneza website na kuposti vitu mbalimbali.