The House of Favourite Newspapers
gunners X

Meridianbet Yatoaa Vifaa vya Michezo kwa Amani Jogging Vingunguti

0

Katika muendelezo wa ubunifu na utofauti wake, Meridianbet imezidi kuthibitisha kuwa haijajikita tu katika kutoa burudani ya kipekee ya michezo ya kubashiri na kasino mtandaoni, bali pia ni mshirika halisi wa maendeleo ya jamii. Kupitia programu yake ya uwajibikaji wa kijamii (CSR), Meridianbet imefanya tukio la kugusa moyo wa wengi, kugawa vifaa vya michezo kwa kikundi cha Amani Jogging kilichopo Vingunguti, Jijini Dar es Salaam.

Tukio hili lilijaa furaha na mshikamano, ambapo wanachama wa Amani Jogging walipokea jezi na mipira ya kisasa, hatua inayolenga kuhamasisha vijana na watu wazima kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za michezo na mazoezi ya mwili. Kupitia mpango huu, Meridianbet inaendeleza azma yake ya kuchochea maendeleo ya michezo kama nyenzo ya afya, umoja na ustawi wa jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa Meridianbet alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuinua michezo ya jamii akisema:

“Tunatambua umuhimu wa michezo katika kuleta afya, umoja na kuimarisha mahusiano ya kijamii. Ndiyo maana Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vikundi vya michezo vya jamii, ili kuhakikisha kila kijana na mwanajamii ana nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za michezo kwa urahisi zaidi. Tunahamasisha vijana wote kuendelea kutumia muda wao vizuri katika michezo na kujiepusha na vitendo visivyo na tija.”

Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni ili kupata ushindi kirahisi zaidi. Pia, ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo yenye ODDS KUBWA ZAIDI!.  PIGA *149*10# au tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Kwa upande mwingine, kiongozi wa Amani Jogging alionyesha shukrani za dhati kwa Meridianbet kwa mchango huo wa thamani, akisema:

“Tunaishukuru sana Meridianbet kwa kutuona sisi wana Vingunguti. Vifaa hivi vitatusaidia sana kuendelea na mazoezi yetu kwa ari zaidi. Ni nadra kupata wadau wanaotambua juhudi za vikundi vya michezo vya jamii kama sisi, na kwa hili tunasema asanteni sana.”

Zaidi ya kuwa kasino ya kisasa yenye ubunifu na teknolojia ya hali ya juu, Meridianbet imeendelea kujitambulisha kama nembo ya mabadiliko chanya katika jamii. Kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya kijamii inayogusa sekta za afya, elimu, michezo, na mazingira, ikiweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa Watanzania.

Kupitia kaulimbiu yake, “Meridianbet – Tunacheza Pamoja na Jamii,” kampuni inabaki kuwa mfano wa kuigwa kwa kuonyesha kuwa michezo na burudani vinaweza kuwa chanzo cha matumaini, afya, na maendeleo chanya katika jamii.

Leave A Reply