
David Beckham Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya England ametawazawa kwa kupewa Medali ya Sir kwenye Sherehe huko Berkshire.
Sir David Beckham alitunukiwa Medali hiyo kwa kutambua mchango wake bora katika soka na jamii ya Waingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye alichezea klabu zikiwemo Manchester United na Real Madrid, aliichezea nchi yake mechi 115 na kuwa Nahodha wa ‘Three Lions’ kwa miaka sita kati ya 2000 na 2006.

Beckham alishiriki Kombe la Dunia akiwa na England mara tatu huku akicheza michuano ya Uropa mara mbili.
Amefanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
Watoto (UNICEF) tangu 2005, na mwaka 2015 mfuko ulianzishwa kwa jina lake kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya ushirikiano.
Pia ni Mmiliki wa Inter Miami, mojawapo ya timu zinazocheza Ligi ya nchini Marekani (Major League Soccer).