
Wachezaji wa timu ya Arsenal wakiwa katika hekaheka za kuwania mpira na wachezaji wa Swansea City usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Emirates. Arsenal imefungwa 2-1.

Williams Wheels wa Swansea akishangilia baada ya kufunga bao la pili dakika ya dakika ya 74 kipindi cha pili.

Mchezaji wa Arsenal, Nacho Monreal baada ya mechi.

Kipa wa Swansea City, Lukasz Fabiansk akishangilia baada ya mechi kuisha.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa katika pozi tofauti baada ya timu yake kufungwa.
Matumaini ya Arsenal kutwaa taji la Ligi Kuu ya England (Premier) kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12, yamezidi kufifia baada ya jana kufungwa 2-1 na Swansea City kwenye uwanja wa nyumbani, Emirates.
Arsenal walikuwa wakiongoza, kupitia bao la Joel Campell na ilionekana kana kwamba wangepunguza tofauti kati yao na vinara, Leicester City lakini mambo yalibadilika ghafla. Swansea, waliokuwa bila meneja wao, Francesco Guidolin, walisawazisha kupitia kwa Wayne Routledge.
Olivier Giroud na Alexis Sanchez waligonga mwamba wa goli lakini bahati haikuwa upande wao. Ashley Williams alilizamisha jahazi la Arsenal baada ya kuifungia Swansea bao la pili na la ushindi lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo, matokeo yakiwa 2-1.
Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa Jumatano usiku:
- Arsenal 1-2 Swansea
- Stoke 1-0 Newcastle
- West Ham 1-0 Tottenham
- Liverpool 3-0 Man City
- Man Utd 1-0 Watford