×

Man City Yaibuka na Ushindi wa Mabao 5–4 Dhidi ya Fulham

Manchester City imeondoka na pointi tatu muhimu baada ya kuibuka na ushindi wa 5–4 dhidi ya Fulham katika mchezo wenye msisimko mkubwa uliochezwa katika dimba la Craven Cottage.

Mtanange huo uliokuwa na jumla ya mabao tisa ulitoa burudani ya hali ya juu, huku timu zote zikionesha uwezo mkubwa wa kushambulia. Ushindi huo unaifanya Manchester City kufikisha alama 28 na kusalia nafasi ya pili baada ya mechi 14 za Ligi Kuu England, wakati Fulham ikisalia nafasi ya 15 na alama 17.

Jinsi Magoli Yalivyofungwa – Fulham 4–5 Man City
Magoli ya Fulham

⚽ 45+2’ – Emile Smith Rowe: Alipunguza tofauti kabla ya mapumziko kwa kumalizia kwa ustadi.

⚽ 57’ – Alex Iwobi: Akapachika bao la pili akiimaliza vyema pasi ya ndani ya kijisanduku.

⚽ 72’ – Samuel Chukwueze: Akawapa wenyeji matumaini kwa mkwaju mzuri uliomzidi kipa Ortega.

⚽ 78’ – Chukwueze: Akaongeza la nne na kuifanya mechi kuwa yenye presha kubwa hadi dakika za mwisho.

Magoli ya Manchester City

⚽ 17’ – Erling Haaland: Alifungua ukurasa wa mabao katika mchezo huo.

⚽ 37’ – Tijjani Reijnders: Akaongeza la pili kwa shuti la nje ya boksi.

⚽ 44’ – Phil Foden: Akaweka bao la tatu kabla ya mapumziko.

⚽ 48’ – Phil Foden: Akaanza kipindi cha pili kwa kasi, akitupia la nne kwa City.

⚽ 54’ – Sander Berge (og): Shinikizo la mashambulizi ya City likamsababisha mchezaji wa Fulham kujifunga.

Licha ya Fulham kupambana mpaka mwisho, City walidumu na uongozi hadi filimbi ya mwisho.

Matokeo Mengine EPL

Bournemouth 0–1 Everton

⚽ 78’ – Jack Grealish: Bao lake lilitosha kuiwezesha Everton kurudi nyumbani na ushindi muhimu.

KESI KUPINGA TUME ya RAIS MAHAKAMA YATOA SIKU 7/ALIYEBAKWA na DAKTARI AFUNGUKA-YEYE AFUKUZWA

Leave a Comment