The House of Favourite Newspapers
gunners X

CEOrt na IUCN Waunganisha Nguvu Kuleta Mapinduzi ya Kijani Sekta ya Utalii

0

Arusha, Tanzania – Jukwaa la Wakurugenzi wa Makampuni nchini (CEOrt Roundtable), kwa kushirikiana na Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) na wadau muhimu wa utalii, limeandaa Warsha ya Ngazi ya Juu ya kuhamasisha matumizi ya njia za asili (Nature-based Solutions (NbS) jijini Arusha katika mnyororo mzima wa thamani wa utalii nchini Tanzania ili kupambana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika sekta hiyo hapa nchini.

Kikao hicho kiliwaleta pamoja wataalamu wa uhifadhi, wadau wa sekta binafsi, taasisi za utafiti, na wawakilishi wa mashirika ya umma wanaoshughulika na utekelezaji na uendeshaji wa ajenda ya nchi ya uendelevu na ustahimilivu wa tabia nchi.

Warsha hiyo, iliyoratibiwa na wataalamu akiwamo Dkt. Mike Musgrave kutoka kampuni ya New Natural Capital, Dkt. Gileard Minja, na Dkt. Nyanjige Mayala kutoka Sustainable Tourism Tanzania (STTZ), iliongelea namna ya urejeshaji wa mandhari za kimazingira, ulinzi wa vyanzo vya maji, upanuzi wa uhifadhi wa wanyamapori unaoongozwa na jamii, na uwekezaji katika mifumo ya ikolojia ya kaboni ya buluu ‘blue carbon’ vinavyoweza kuimarisha ushindani wa utalii wa Tanzania sambamba na kuendeleza viwango vya mazingira, jamii na utawala bora (ESG).

Kupitia Nguzo yake ya Biashara na Uendelevu, CEOrt inaendelea kuiweka sekta binafsi kama injini muhimu mabadiliko ya kijani nchini Tanzania. Kupitia Mradi wa Resolve NBS, unaofadhiliwa na NORAD na kutekelezwa kwa ushirikiano na IUCN, juhudi za CEOrt zinalenga Kuwezesha biashara kupitia mwongozo wa vitendo, mifano halisi ya utekelezaji na kutoa maarifa ya kifedha , Ili kujumuisha Suluhisho Zinazotokana na Asili katika mikakati ya uendelevu wa makampuni na maamuzi ya uwekezaji.

“Utalii ni moja ya sekta zinazotegemea sana mazingira nchini Tanzania,” alisema Hawa Urungu, Meneja wa Miradi CEOrt. “Tukilinda mazingira, tunalinda masoko yetu. NbS zinatoa njia madhubuti kwa waendeshaji utalii kupunguza hatari za tabianchi, kuimarisha ustahimilivu wa vivutio vyetu, na kukidhi matarajio ya kimataifa ya uendelevu. Hii si ajenda ya mazingira pekee—ni ajenda ya ushindani wa kibiashara.”, amesema.

Washiriki walibainisha fursa zinazoibuka katika mifumo ya uhifadhi shirikishi, urejeshaji wa mifumo ya ikolojia ya ukanda wa Pwani, kilimo bunifu na endelevu kwa minyororo ya ugavi wa hoteli, na miundombinu ya utalii .

Majadiliano yalisisitiza pia kuwa ujumuishaji wa NbS unaweza kuboresha huduma wa watalii, kulinda urithi wa taifa, na kufungua vyanzo vipya vya uwekezaji wa kijani, hasa wakati ambapo wasafiri wa kimataifa wanapendelea kutembelea maeneo yenye athari chanya kwa mazingira.

Licha ya maendeleo mazuri, wadau walisisitiza hitaji la msaada zaidi wa kitaalamu, ufadhili mahsusi, na sera wezeshi. Baadhi ya kampuni za utalii zilionyesha utayari wa kupanua miradi ya NbS lakini zikataja changamoto za ukosefu wa motisha, gharama kubwa za awali, na uratibu hafifu wa taasisi kama vikwazo vinavyojirudia.

Warsha ilihitimishwa kwa wito mmoja wa pamoja: ili kusambaza kwa mafanikio matumizi ya NbS katika sekta ya utalii ya Tanzania, inahitajika ushirikiano endelevu kati ya serikali, taasisi za kifedha, na sekta binafsi.

Utolewaji wa hamasa, ukuaji wa vyombo vya kifedha na uimarishaji wa uwezo wa ndani ni muhimu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki kuwa moja ya maeneo bora duniani, yenye utajiri wa maliasili na yanayoweza kustahimili shinikizo la tabianchi na masoko.

Kadiri Tanzania inavyoendelea kuelekea malengo yake ya maendeleo ya muda mrefu na Dira ya 2050, Suluhisho Zinazotegemea Njia za Asili yanajidhihirisha kama nyenzo muhimu ya kulinda uadilifu wa mazingira na ustawi wa uchumi.

Mwitikio na kasi iliyojengwa kupitia ushirikiano wa CEOrt–IUCN ni hatua muhimu kuelekea utekelezaji wa vitendo—ikihakikisha kuwa sekta ya utalii inachangia kikamilifu katika uchumi unaohifadhi mazingira, unaostahimili tabianchi, na unaoweza kushindana kimataifa.

Leave A Reply