The House of Social Media
gunners X

PSRS Yatangaza Nafasi 208 za Ajira Serikalini Taasisi 10 Mbalimbali

0

Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza jumla ya nafasi 208 za ajira katika taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali kwa niaba ya waajiri, ikiwemo TAWA, TASAC, NBS, TIRA, TAFORI, CAMARTEC, CBE, TCAA, NIC na CAWM.

Tangazo hilo limetolewa rasmi tarehe 10 Januari, 2026, likiwaalika Watanzania wenye sifa, uadilifu na ari ya kufanya kazi kuomba nafasi hizo kupitia Ajira Portal.

BONYEZA HAPA KUSOMA >>> NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 

Taasisi Zilizotangaza Ajira

Ajira hizo zinahusisha taasisi zifuatazo:

  • Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA)

  • Tanzania Shipping Agency Corporation (TASAC)

  • National Bureau of Statistics (NBS)

  • Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA)

  • Tanzania Forestry Research Institute (TAFORI)

  • Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology (CAMARTEC)

  • College of Business Education (CBE)

  • Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA)

  • National Insurance Corporation (NIC)

  • College of African Wildlife Management (CAWM)

Aina za Nafasi Zilizotangazwa

Nafasi zilizotangazwa zinahusisha kada mbalimbali zikiwemo:

  • Wahifadhi na Askari Uhifadhi (Conservation Rangers)

  • Madereva, Mafundi Mitambo na Mafundi Maabara

  • Wataalamu wa Takwimu, TEHAMA na Programu (ICT Officers, Statisticians)

  • Maafisa Bima, Uhasibu na Takwimu

  • Wahadhiri Wasaidizi na Wasaidizi wa Mafunzo

  • Wataalamu wa Anga, Usafiri wa Majini na Uhandisi

  • Watafiti wa Misitu, Ufugaji Nyuki, Entomolojia, Microbiology na Botania

Ajira hizo zinahusu ngazi za Cheti, Stashahada, Shahada ya Kwanza, Shahada ya Uzamili hadi kada za kitaaluma za juu.

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

Kwa mujibu wa PSRS:

  • Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania

  • Umri usizidi miaka 45, isipokuwa kwa taasisi za kijeshi na ulinzi

  • Waombaji waliopo katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

  • Waombaji waliostaafu hawaruhusiwi kuomba

  • Waombaji wanatakiwa kuambatanisha vyeti halisi vilivyothibitishwa, cheti cha kuzaliwa na picha ya pasipoti

  • Vyeti vya nje ya nchi lazima vitambuliwe na TCU, NACTVET au NECTA

Namna ya Kutuma Maombi

Maombi yote yanapaswa kutumwa mtandaoni pekee kupitia:
👉 http://portal.ajira.go.tz

Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine hayatazingatiwa.

Mwisho wa Kutuma Maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 24 Januari, 2026.

BONYEZA HAPA KUSOMA >>> NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 

Leave A Reply