Dkt. Mwigulu Akutana Na Prof. Mkenda Na Timu Ya Wataalam Ya Wizara Ya Elumu
Waziri Mkuu, Dkt.Mwigulu Nchemba leo Januari 15, 2026 amefanya kikao cha kazi na Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, pamoja na Timu ya Wataalam kutoka Wizara hiyo.
Kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma pamoja na mambo mengine wamejadili mikakati mbalimbali yenye lengo la kuendeleza sekta ya elimu nchini.
Katika kikao hicho pia, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo alishiriki.


