×

Moto Mkubwa Wazuka katika Jengo la NSSF Dar – Video

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa moto mkubwa umezuka katika Jengo la Ghorofa National Social Security Fund (NSSF) lililopo karibu na Mnara wa Askari, Posta jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji tayari limewasili na linaendelea kuchukua hatua za kuuzima moto huo.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu chanzo cha moto huo wala athari zake, ikiwemo majeruhi au uharibifu wa mali.

Kwa taarifa zaidi na maendeleo ya tukio hili, endelea kufuatilia GLOBAL TV.

Video full ipo YouTube ya Global TV

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave a Comment