×

Prof. Shemdoe Aishukuru Nmb Kwa Kutoa Msaada wa Vifaa Tiba Na Vya Elimu Lushoto

 

MCHANGO WA NMB LUSHOTO WAINUA SEKTA YA AFYA NA ELIMU -pesatu.co.tz
Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameishukuru Bank ya NMB kwa kutoa mchango wa vifaa tiba na vya elimu jimboni Lushoto, vifaa ambavyo vitaongeza ufanisi katika eneo utoaji wa elimu na huduma za afya msingi kwa wananchi jimboni kwake.
Shukrani hizo za Prof. Shemdoe zimetolewa na mratibu wa shughuli za jimbo Mwalimu Catherine Singano kwa niamba ya Prof. Shemdoe, wakati wa hafla ya kupokea msaada huo vya vifaa tiba na vya elimu iliyofanyika Januari 19, 2026 Lushoto
MCHANGO WA NMB LUSHOTO WAINUA SEKTA YA AFYA NA ELIMU -pesatu.co.tz
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 56,000,000/= vimekabidhiwa leo na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Bw. Ladislaus Baraka kwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Sephania Sumaye kwa ajili ya kupelekwa Hospitali ya Lutheran ya Lushoto, Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, shule za sekondari za Ngulwi, Migambo na Kiniko pamoja na shule za msingi za Ndeme, Chumbageni na Bombo.
Mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Bw. Ladislaus Baraka alisema kuwa, Benki ya NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za jamii hususani katika kuboresha huduma za Elimu na Afya nchini.
MCHANGO WA NMB LUSHOTO WAINUA SEKTA YA AFYA NA ELIMU -pesatu.co.tz
Aidha, Bw. Baraka amempongeza na kumshukuru Mbunge wa Lushoto Prof. Riziki Shemdoe kwa jitihada zake za kuishawishi Benki ya MNB kujitolea vifaa tiba na vifaa vya elimu katika shule na hospitali zilizopo jimboni kwake, kitendo ambacho kimepelekea benki hiyo kuona umuhimu wa kuchangia vifaa hivyo ili kuboresha utoaji wa huduma za afyamsingi na elimu msingi wilayani Lushoto.
Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Sephania Sumaye ameishukukuru Benki ya NMB kwa msaada huo walioutoa na kipekee amemshukuru Mbunge wa Lushoto Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, kwa kuendeleza jitihada zake za kuwashawishi wadau wa maendeleo kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu na afya msingi.
MCHANGO WA NMB LUSHOTO WAINUA SEKTA YA AFYA NA ELIMU -pesatu.co.tz
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 56,000,000/= vilivyotolewa na Benki ya NMB jimboni lushoto, ni Vitanda vya kulazia wagonjwa, magodoro, mashuka, madawati, viti, meza na mabati.

Leave a Comment