
Meridianbet imeendelea kudhihirisha kuwa ni zaidi ya kampuni ya michezo ya kubahatisha kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, Meridianbet ilikabidhi vifaa mbalimbali vya usafi na kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, lengo likiwa ni kuboresha hali ya usafi na afya ya jamii.
Katika hatua ya kuimarisha mapambano dhidi ya uchafu na magonjwa yatokanayo na mazingira machafu, Meridianbet ilitoa msaada wa vifaa muhimu vya usafi ikiwemo mifagio, mafyekeo, koleo, glovu, mifuko ya taka pamoja na viatu vya kufanyia usafi. Msaada huu ulilenga kuwawezesha wakazi wa Mbezi Juu kuwa na zana za kutosha za kufanyia usafi kwa muda mrefu.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Kutoka Meridianbet, mwakilishi wa kampuni hiyo, Nancy Ingram alieleza ni kwa namna gani kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha jamii inakua kwenye mazingira safi na salama ili kuepuka magonjwa ya milipuko ambayo yamekua yakiikumba jamii.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Diwani wa Kata ya Mbezi Juu aliipongeza Meridianbet kwa kuonesha mfano wa kuigwa kwa kushirikiana na serikali za mitaa katika kulinda mazingira. Ushirikiano huu umeelezwa kuwa ni nguzo muhimu ya kuleta mabadiliko ya kudumu, kwani unachochea uwajibikaji wa pamoja kati ya sekta binafsi, viongozi na wananchi katika kulinda afya ya jamii.
Kupitia kampeni hii, Meridianbet imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii yenye matokeo chanya kwa jamii. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa mazingira safi ni msingi wa maisha bora na maendeleo endelevu, hivyo itaendelea kushirikiana na jamii.
