Mzee Tifutifu Anayedai Kuwatupia Majini Simba Afunguka – Video

Mzee Athuman Mshomari almaarufu Mzee Tifutifu, ambaye anadai kuwa ni mganga wa kienyeji, amedai kuwa yeye ndiye chanzo cha matokeo mabaya yanayoikumba Klabu ya Simba, ikiwemo kufungwa mara kwa mara na kushuka kwa kiwango cha uchezaji wa baadhi ya wachezaji wake.
Amesema anayo madai yake kwa viongozi wa klabu hiyo na kwa sababu walikataa kuyatekeleza, aliamua ‘kuitupia majini’, akisisitiza kuwa Simba haitaweza kupata mafanikio hadi viongozi wa klabu hiyo watakapofika kuzungumza naye.
Aidha, amedai kuwa kuna mambo muhimu yanayohitaji kujadiliwa kati yake na viongozi wa klabu hiyo kabla ya hatua zozote kuchukuliwa.

