
Waziri wa fedha na mipango Zanzibar Dkt Juma Malik Akili amesema serikali ya mapinduzi Zanzibar inatambua mchango wa sekta za kifedha katika maendeleo ya nchi na kukuza uchumi wa kukuza uchumi wa Zanzibar hivyo ni vyema sekta hizo kuongeza mashirikiano katika miradi mikubwa ya maendeleo.
Ni wakati akizungumza na wadau wa KCB benki katika iftar ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo waziri wa fedha na mipango Dkt Juma Malik Akilii amesema maendeleo ya Zanzibar inakua kwa kujengwa na watanzania na washirika wa maendeleo.

Mkuu wa kitengo cha KCB Sahil benki Amour Muro amesema benki hiyo ni mshirika wa serikali katika kupunguza umaskini na mdau wa maendeleo katika sekta za elimu, afya , mazingira na ujasiriamali ambapo wanaamini benki ina jukumu la kusaidia jamii.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya KCB shariah Sheikh Khamis Mataka ya amesema mwezi mtukufu wa ramadhan unakumbusha kufanya biashara kwa uadilifu, uwazi na kumcha mwenyezi Mungu ndo mana benki hiyo ilianzisha na kuendendelea kuimarisha huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya sharia.
Iftar hiyo ilihudhuriwa na wateja wa benki ya KCB sambamba na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha