
Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea rasmi baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu pambano kali kati ya Simba SC na Coastal Union leo Aprili 2, 2026
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Stadium majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Simba wanaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, huku ikiwa na rekodi bora ya ushindi dhidi ya wapinzani wao katika mechi 23 walizokutana.
Kwa upande wa Coastal Union, wanahitaji matokeo mazuri ili kuboresha nafasi yao na kuvunja historia mbaya wanapokutana na Simba
- Simba SC wameshinda mechi 16
- Coastal Union wameshinda 1
- Sare zikiwa 6
Hii inaonyesha ubabe wa Simba kwenye mchezo huu.
Matokeo ya Mechi Zilizopita
- 01/03/2025: Coastal Union 0-3 Simba SC
- 04/10/2024: Simba SC 2-2 Coastal Union
- 09/03/2024: Coastal Union 1-2 Simba SC
- 21/09/2023: Simba SC 3-0 Coastal Union
- 09/06/2023: Simba SC 3-1 Coastal Union
- 03/12/2022: Coastal Union 0-3 Simba SC
- 07/04/2022: Coastal Union 1-2 Simba SC
- 31/10/2021: Simba SC 0-0 Coastal Union
- 11/07/2021: Simba SC 2-0 Coastal Union
- 21/11/2020: Coastal Union 0-7 Simba SC
SOMA HII ZAIDI>> Dakika 1 Tu Inaweza Kukupa Utajiri! Jaribu Live In-Play Booster Leo
Hii hapa ratiba ya mechi zijazo kwa Simba
Azam FC vs Simba SC, Aprili 5,2026 saa 1:00 usiku
Fountain Gate FC vs Simba SC, Aprili 9, 2026, saa 10:00 jioni
Namungo FC vs Simba SC, Aprili 15,2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs JKT Tanzania, Aprili 19,2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs Tanzania Prisons, Aprili 29, 2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2026 saa 11:00 jioni.
Mashujaa FC vs Simba SC, saa 12:15, jioni.
Coastal Union vs Simba SC, Mei 16,2026 saa 10:00 jioni
Simba SC vs Dodoma Jiji FC, Mei 20,2026, saa 1:00 usiku.